TraceKwao ni mfumo wa kitaifa wa kidijitali unaolenga kusaidia kutambua, kufuatilia na kuwaunganisha watoto waliopotea na familia zao kwa kutumia teknolojia ya kisasa.
TraceKwao ni mfumo wa kitaifa wa kidijitali unaolenga kusaidia kutambua, kufuatilia na kuwaunganisha watoto waliopotea, waliotelekezwa, waliokimbia nyumbani, waliopatikana bila uangalizi wa wazazi au walezi, pamoja na watu wazima waliopatikana wakiwa hawajulikani au wasioweza kutambua familia zao.
Mfumo huu unatumia teknolojia ya kisasa pamoja na ushirikiano wa taasisi mbalimbali ili kuhakikisha kuwa kila mtoto au mtu aliyepotea anapata fursa ya kurejea salama kwa familia yake, mlezi halali au mazingira salama yanayostahili.
Kupitia TraceKwao, wananchi, Jeshi la Polisi, maafisa ustawi wa jamii, hospitali, vituo vya afya, shule, vituo vya kulelea watoto, mamlaka za serikali za mitaa, mashirika yasiyo ya kiserikali pamoja na wadau wengine wanaweza kuripoti matukio ya watoto waliopotea au waliopatikana na kushirikiana katika kuwatafuta, kuwatambua na kuwaunganisha na familia zao.
Kuwa mfumo wa kitaifa unaoongoza nchini Tanzania katika kulinda watoto na kuwaunganisha kwa haraka, salama na kwa ufanisi watoto waliopotea pamoja na watu wengine walio katika mazingira hatarishi na familia zao.
Kutumia teknolojia ya kisasa, ushirikiano wa wadau na usimamizi salama wa taarifa katika kurahisisha utoaji wa taarifa, utambuzi, ufuatiliaji na uunganishaji wa watoto waliopotea na watu walio katika mazingira hatarishi na familia zao nchini Tanzania.
TraceKwao hutoa mfumo salama wa kidijitali unaowezesha:
Ripoti haraka kwa kutumia mfumo wa kidijitali
Andika taarifa za mtoto aliyepatikana
Watu wazima waliopatikana hawajulikani
Mchakato mzima hadi kesi kufungwa
Kati ya taasisi mbalimbali
Kwa kutumia picha na taarifa muhimu
Ya kesi kila kesi kwa wakati halisi
Kuhifadhi taarifa za watoto waliopotea
Taarifa za usimamizi
Kati ya taasisi mbalimbali
Mfumo huu unasaidia ushirikiano kati ya taasisi mbalimbali:
Misingi ya maadili inayotuangazia katika kila tunachofanya
Kila uamuzi unaofanywa unaweka mbele maslahi, usalama na utu wa mtoto.
Tunazingatia uaminifu, uwajibikaji na weledi katika kila huduma tunayotoa.
Tunalinda taarifa binafsi kwa kutumia mifumo salama ya kidijitali na udhibiti wa upatikanaji wa taarifa.
Tunaamini kuwa mafanikio ya kuwaunganisha watoto na familia zao yanategemea ushirikiano kati ya serikali, taasisi, jamii na familia.
Tunatumia teknolojia na mbinu bunifu kuboresha huduma zetu kila wakati.
Kila mtoto aliyepotea ni tumaini la familia linalostahili kurejeshwa nyumbani salama.
Malengo yanayotupambazia katika kutekeleza dhima yetu
Kupunguza idadi ya watoto wanaopotea bila kupatikana.
Kuimarisha mfumo wa taifa wa ulinzi wa mtoto.
Kuboresha ushirikiano kati ya taasisi zinazohusika.
Kuharakisha uunganishaji wa watoto na familia zao.
Kujenga na kusimamia kanzidata salama ya kitaifa.
Kuboresha maamuzi kupitia takwimu na uchambuzi wa taarifa.
Kuelimisha jamii kuhusu ulinzi wa mtoto na umuhimu wa kuripoti matukio kwa wakati.
Kuwaunganisha kila mtoto aliyepotea na familia yake kwa salama.
TraceKwao imejizatiti kulinda haki za watoto, kuhifadhi usiri wa taarifa binafsi na kuhakikisha kila tukio linaloripotiwa linashughulikiwa kwa wakati kupitia ushirikiano wa taasisi husika.
Kila mtoto anastahili ulinzi. Kila familia inastahili matumaini. Kila muungano wa familia una thamani.
"Kuunganisha Familia Kupitia Teknolojia."